1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mchakato wa katiba ya Umoja wa Ulaya uendelezwe

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6y

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani na Rais Jaques Chirac wa Ufaransa wameyataka mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya kuendelea na kuidhinisha katiba ya umoja huo licha ya kukataliwa na wapiga kura wa Ufaransa na Uholanzi.

Mazungumzo yao yaliodumu kwa masaa mawili mjini Berlin hapo jana wakati wa chakula cha usiku yalilenga hali ngumu inayoikabili Umoja wa Ulaya kufuatia kukataliwa kwa katiba ya Umoja huo katika kura za maoni za taifa nchini Ufaransa na Uholanzi wiki iliopita.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Ujerumani Bela Anda viongozi hao ambao wamekutana kujadili msimamo wao kabla ya mkutano ya viongozi wa Umoja wa UIaya baadae mwezi huu wamekubalina kwamba mchakato wa kuidhinisha katiba hiyo lazima uendelee ili kwamba maoni ya kila nchi yaweze kuheshimiwa.

Suala hilo linatarajiwa kuhodhi mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya uliopangwa kufanyika mjini Brussels tarehe 16 na 17 mwezi huu.

Nchi 10 za Umoja wa Ulaya zenye kuwakilisha kama nusu ya idadi ya watu wa Umoja wa Ulaya hivi sasa zimeidhinisha katiba hiyo lakini kukataliwa kwake na nchi mbili waasisi wa umoja huo kumezusha mashaka iwapo katiba hiyo bado inaweza kuwepo.