1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mazungumzo ya Umoja wa Ulaya na Iran kuendelea

28 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD8D

Mazungumzo mjini Berlin kati ya Umoja wa Ulaya na Iran kuhusu mpango tata wa nuklea wa Iran yamekatizwa wakati wa usiku lakini yanatarajiwa kuanza tena leo hii.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Havier Solana na msuluhishi mkuu wa mzozo huo wa nuklea wa Iran Ali Larijani wanajaribu kuyakinisha iwapo kuna msingi wa kuendelezwa kwa mazungumzo hayo.Hadi sasa kumefanyika mikutano miwili ya aina hiyo mwezi huu kuelezea mpango wa kuishaijisha Iran isitishe urutubishaji wa uranium.

Mpango huo wa vifuta jasho vya kiuchumi na kisiasa umependekezwa na Marekani,Russia,China,Ufaransa,Uingereza na Ujerumani.

Hadi sasa Iran imekuwa ikikataa wito wote iliokuwa ikitolewa na Umoja wa Mataifa kutaka iachane na mpango wake huo wa nuklea ambao mataifa ya magharibi wanaushuku kuwa ni kwa ajili ya kutengeneza silaha za nuklea.

Akizungumza mjini Tehran hapo jana Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amesisitiza tena kwamba Iran iko wazi kwa mazungumzo lakini haitokubali kuridhia haki zake za nuklea na kupuuza sheria ya Mkataba wa Kuzuwiya Kuenea kwa Silaha za Nuklea.