1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN Mahakama kuu ya Ujerumani kuamua juu ya waranti za umoja wa Ulaya

18 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtU

Mahakama kuu nchini Ujerumani inajiandaa kupitisha uamuzi ikiwa waranti za umoja wa Ulaya ni za kisheria. Uhalali wa waranti hizo umetiliwa shaka na raia wa Ujerumani mwenye asili ya Syria, Mamoun Darkazanli. Jamaa huyo alitiwa mbaroni mjini Hamburg mwaka jana kufuatia waranti ya umoja wa Ulaya iliyotolewa nchini Uhispania.

Maofisa wa Uhispania wanamtaka ajibu mashataka ya ugaidi kwani inaaminiwa kuwa ni mdhamini mkubwa wa mtandao wa kundi la kigaidi la al-Qaeda barani Ulaya. Alitakiwa kurudishwa nchini Uhispania lakini mahakama ya sheria ikaipinga hatua hiyo. Mawakili wa Mamoun wamesisitiza kwamba sheria ya Ujerumani inawalinda raia wake dhidi ya kuwarudisha kuhukumiwa katika mataifa walikofanya makosa.

Waranti ya umoja wa Ulaya inalenga kuboresha ushirikiano katika kuwakamata na kuwashtaki watu wanaotuhumiwa kuwa magaidi.