1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Madereva wa treni waendelea kugoma kazi Ujerumani

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImW

Mgomo wa madereva wa treni ukiendelea siku tatu kwa mfululizo nchini Ujerumani,shirika la reli- Deutsche Bahn linasema,huduma zimeathirika zaidi mashariki mwa nchi.Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo,hali ni mbaya zaidi katika usafirishaji wa mizigo.Wakati huduma kadhaa zimeweza kutekelezwa upande wa magharibi,katika mashariki kulikuwepo misafara ya huduma zenye umuhimu mkubwa tu.

Mashariki mwa Ujerumani,madereva wengi wamo katika chama cha wafanyakazi cha madereva wa treni-GDL na wamejiandaa kwa mgomo.GDL kinadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 31.Msemaji wa Deutsche Bahn,Gunnar Meyer amesema,shirika la reli linajitahidi kutenzua mgogoro wa madereva.

Waziri wa Usafiri,Wolfgang Tiefensee ametoa mwito kwa pande zote mbili kurejea kwenye meza ya majadiliano,mgomo wa sasa utakapomalizika Jumamosi asubuhi.