1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kodi ya VAT kuongezeka nchini Ujerumani.

5 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELq

Kodi ya thamani ya ongezeko la bei VAT nchini Ujerumani inaweza kupanda hadi kufikia asilimia 20.

Katika mahojiano katika televisheni , kiongozi mteule wa chama cha Social democrats Matthias Platzeck amesema kuwa uwezekano wa ongezeko la kodi ya thamani ya ongezeko la bei, VAT kutoka asilimia 16 ya sasa hadi 20 ni suala linalowezekana. Amesema kuwa punguzo katika bajeti ni suala la lazima na kwamba maamuzi magumu yanaweza kutarajiwa. Tangazo hilo linakuja wakati wizara ya fedha mjini Berlin imetoa mapitio mapya kuhusu utabiri wake wa mapato ya kodi kwa mwaka huu na mwaka ujao.