1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kiongozi wa SPD , awa makamu wa kansela.

14 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESD

Nchini Ujerumani , kiongozi wa chama cha Social Democrats, Franz Muentefering ameteuliwa kuwa makamu wa kansela na waziri wa kazi katika serikali ya mseto chini ya kansela mtarajiwa wa chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union , Angela Merkel.

Wizara ya fedha itachukuliwa na Peer Steinbrueck , waziri mkuu wa zamani wa chama cha SPD katika jimbo la North Rhine Westphalia.

Frank – Walter Steinmeier anachukua nafasi ya Joschka Fischer kama waziri wa mambo ya kigeni.

Chama cha Social Democrats kitaendesha wizara nane kati ya 14 katika serikali ya mseto katika kile kinachojulikana kama muungano mkuu.

Chama cha kihafidhina cha Angela Merkel cha CDU kitakuwa na wizara 6.

Wizara ya uchumi itakwenda kwa chama ndugu cha Bibi Merkel cha CSU na kiongozi wake Edmund Stoiber ndie atakuwa waziri wa uchumi.