1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan anatazamiwa kuwasili ...

11 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFt6
Ujerumani hii leo kwa ziara rasmi mjini Berlin.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amepangiwa kuzungumza na kansela Gerhard Schröder,waziri wa mambo ya nchi za nje Joschka Fischer,mwenyekiti wa achama cha upinzani cha CDU bibi Angela Merkel na rais wa shirikisho Johhanes Rau.Mazungumzo yao yatahusiana na hali nchini Afghanistan,mashariki ya kati na jukumu la Umoja wa mataifa katika kuimarisha amani nchini Iraq.Juhudi za kuifanyia marekebisho jumuia hiyo ya kimataifa ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa wakati wa aziara ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan nchini Ujerumani.Kesho Kofi Annan atachambua jukumu la siku za mbele la umoja wa mataifa mbele ya wasomi na wanafunzi wa chuo kikuu cha Tübingen.