1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amewasili mjini Berlin ...

11 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFt0
kwa ziara rasmi nchini Ujerumani hii leo.Amekua na mazungfumzo pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje Joschka Fischer.Kiini cha mazungumzo yao ni kuhusu juhudi za kuimarisha hali ya utulivu nchini Afghanistan,mashariki ya kati na juhudi za kuufanyia marekebisho umoja wa mataifa.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amepangiwa pia kuonana na kansela Gerhard Schröder , rais wa shirikisho bwana Johannes Rau na mwenyekiti wa chama cha CDU bibi Angela Merkel.Kesho katibu mkuu Annan atachambua jukumu la siku za mbele la Umoja wa mataifa mbele ya wasomi na wanafunzi wa chuo kikuu cha Tübingen.