1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela wa Ujerumani ziarani Poland

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIi

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani leo anaanza ziara ya siku mbili nchini Poland.Ziara ya Merkel,imegubikwa na migogoro inayohusika na Katiba ya Umoja wa Ulaya na mradi wa Marekani wa kutaka kuweka Mashariki ya Ulaya roketi za kujikinga dhidi ya makombora.Serikali ya Poland inaupinga mpango wa Kansela Merkel wa kutaka kuwa na Katiba ya Ulaya ifikapo mwaka 2009.kwa upande mwingine,Merkel ameishutumu Poland kwa kuiruhusu Marekani kuweka roketi zake,bila ya suala hilo kupigiwa kura katika Shirika la Kujihami-NATO. Merkel hivi sasa ameshika wadhifa wa urais katika Umoja wa Ulaya.