1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kansela wa Ujerumani atetea msimamo wake wa kutaka China iondolewe vikwazo vya silaha na jumuiya ya Ulaya.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFN8

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder kwa mara nyingine tena ametetea msimamo wake wa kuondoa vikwazo vya silaha vya jumuiya ya Ulaya dhidi ya China. Akilihutubia bunge leo Bwana Schroeder amesema kuwa vikwazo hivyo havina tena umuhimu kutokana na hali ya sasa ya mabadiliko ya kisiasa na kijamii nchini China.

Msimamo wake huo unatatanisha na wengi kati ya wanachama wa chama chake cha Social Democrats wanapinga kuondolewa kwa vikwazo hivyo. Waziri wa mambo ya kigeni Joschka Fischer, mwanachama wa chama kidogo kinachounda muungano wa serikali ya sasa cha Green, amesema kuwa China inahitaji kupiga hatua zaidi kabla ya kupatikana msimamo wa pamoja wa jumuiya ya Ulaya wa kuondoa vikwazo hivyo. Vikwazo hivyo vya silaha viliwekwa kufuatia serikali ya China kupambana na wanafunzi waliokuwa wakidai demokrasia zaidi katika uwanja wa Tianamen mwaka 1989 na kusababisha vifo kadha.