1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kansela wa Merkel asisitiza msimamo wa kuitaka Iran kusitisha urutubishaji madini.

11 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKN

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekiambia kikao cha maafisa wa Ujerumani na Israel mjini Berlin kuwa mataifa makubwa yenye nguvu duniani yanabaki katika msimamo wa kusisitiza kuwa Iran isitishe mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.

Mlango kwa ajili ya majadiliano na Iran bado uko wazi, amesema , lakini si kwa gharama yoyote.

Iran inakana madai ya mataifa ya magharibi kuwa inatengeneza bomu la Atomic na kusema kuwa nia yake ya kujipatia teknolojia ya kinuklia ni kwa matumizi ya amani.

Kansela Merkel pia amekaribisha nia mpya za mataifa ya Kiarabu kusaidia kutatua mzozo kati ya Israel na Palestina, hususan kutoka mataifa manne ambayo ni pamoja na Jordan , Saudi Arabia, UAE na Misr.