1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Fischer na Schroeder kupambana katika mdahalo wa kuiondolea vikwazo vya silaha China.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNN

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder anatarajiwa kutetea uamuzi wake wa kuunga mkono jumuiya ya Ulaya kuondoa vikwazo vya silaha dhidi ya China. Bwana Schroeder ataelezea msimamo wake huo katika bunge la Ujerumani baadaye leo.

Waziri wa mambo ya kigeni Bwana Joschka Fischer pia anatarajiwa kujadili suala hilo bungeni. Anatarajiwa kujiweka mbali na msimamo huo wa Schroeder, kwa kuwa chama chake cha Kijani kimeendelea kuwa msitari wa mbele kutaka vikwazo hivyo viendelee. Vikwazo hivyo viliwekwa kufuatia mauaji ya uwanja wa Tiananmen mwaka 1989.