1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Fischer apinga jeshi la Umoja wa Mataifa kwenda Lebanon

19 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG62

Aliyekuwa zamani waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, amesema itakuwa hatari kubwa kupeleka kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kudumisha usalama nchini Lebanon.

Badala yake Fischer amesisitiza viongozi wenye siasa kali washinikizwe ili watambue umuhimu wa mazungumzo ya kutafuta amani. Fischer ni mtaalamu wa maswala ya Mashariki ya Kati aliyeungwa mkono na wayahudi na wapalestina wakati alipokuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani kwa kipindi cha miaka saba.

Umoja wa Mataifa unataka uruhusiwe kupeleka kikosi kipya cha wanajeshi kwenda Lebanon, kitakochokuwa kikubwa kuliko kikosi cha wanajeshi 2,000 walio katika eneo hilo.

Wakati huo huo, maelfu wa raia nchini Yemen wamefanya maandamano katika mji mkuu Sanaa, kupinga mshambulio ya jeshi ya Israel nchini Lebanon.