1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. CDU kuongeza kodi ya mauzo

11 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvR

Katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani CDU nchini Ujerumani bwana Volker Kauder amesema kwamba kuongeza kaodi ya mauzo itakuwa hatua ya lazima katika juhudi za kupambana na ukosefu wa ajira.

Bwana Kauder amesema ili kutenga nafasi za ajira itakuwa lazima za kuongeza kodi ya mauzo.

Hatahivyo mpango huo unapingwa na chama kingine cha upinzani FDP.

Kiongozi wa chama hicho bwana Wolfgang Gerhardt amesema kwamba inapasa kujaribu kuleta mageuzi katika soko la ajira bila ya kupandisha kodi.

.