1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Azimio la Berlin laidhinishwa na viongozi wa umoja wa ulaya.

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFM

Viongozi wa taifa na serikali wa Umoja wa ulaya, wameidhinisha azimio la Berlin. Waraka huo ni taarifa isiyo zishurutisha nchi wanachama, ikihusiana na maadili na malengo ya siku zijazo. Ulisainiwa na kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye nchi yake ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa ulaya unaozunguka kwa kipindi cha miezi sita miongoni mwa wanachama, pamoja na marais wa halmashauri kuu ya umoja huo na bunge la Ulaya. Tukio hilo ni kilele cha sherehe za mwishoni mwa juma hili mjini Berlin kuadhimisha miaka 50 tangu kusainiwa mkataba wa Roma, ulioweka utaratibu wa hatimae kuundwa umoja wa Ulaya.