1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benzema kutoshiriki michuano ya Kombe la Dunia

20 Novemba 2022

Kufuatia jeraha wakati wa mazoezi, Benzema hatoshiriki michuano hiyo inayoanza leo Jumapili (20.11.2022) huko Qatar

https://p.dw.com/p/4Jn7F
Karim Benzema beim Golden Ball
Picha: Francois Mori/AP/picture alliance

Mwezi mmoja tu baada ya kujishindia tuzo ya mchezaji bora wa kandanda "Ballon d'Or", ndoto ya Karim Benzema ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia inayoanza leo huko Qatar imetoweka baada ya kupata jeraha katika paja lake la kushoto wakati wa mazoezi hapo jana.

Fußball WM Katar | Teamfoto Frankreich
Kikosi cha Timu ya UfaransaPicha: Bertrand Guay/AFP

Timu ya Ufaransa ambao ni mabingwa watetezi, wanakabiliwa na changamoto kubwa baada ya wachezaji wake kadhaa kupata majeraha na hivyo kutoweza kushiriki michuano hiyo muhimu.

UEFA Nations League | Portugal vs. Frankreich | Jubel Frankreich
Picha: Rafael Marchante/REUTERS

Miongoni mwao ni Paul Pogba, N´golo Kante na Christopher Nkunku. Wenyeji Qatar wataingia uwanjani leo jioni kupambana na timu ya Ecuador katika mechi ya ufunguzi kwenye michuano hii ya Kombe la Dunia itakayomalizika Desemba 18.