1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Benki ya Dunia kufadhili miundombinu ya nishati Ukraine

13 Aprili 2023

Benki ya Dinia imesema itatoa kiasi cha dola milioni 200 ili kusaidia kurekebisha miundombinu ya nishati, huku washirika wengine wakitoa kiasi cha dola milioni 300 katika kuutanua zaidi mradi huo.

https://p.dw.com/p/4PzBd
Ukraine Krieg I Lviv - Stromleitung
Picha: Pavlo Palamarchuk/ZUMAPRESS/picture alliance

Ufadhili huo wa dola 200 zitatumika kufanya matengenezo ya dharura katika transfoma, mashine za  kupasha joto za kuhamishika pamoja na vifaa vingine muhimu vya dharura.

Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji wa benk hiyo Anna Bjerde, amesema kiasi cha dola bilioni 23 zimekusanywa kama ufadhili kwa Ukraine na kutokana na miundombinu ya nishati nchini humo kukumbwa na uharibifu wa dola bilioni 11 hivyo kunahitajika msaada wa haraka.

Soma pia: Urusi yazidi kuharibu miundombinu ya Ukraine

Katika miezi ya nyuma Kyiv iliripoti  namna ambavyo vikosi vya Urusi vililenga miundombinu ya nishati ya Ukraine na kusababisha kukatika kwa umeme nchini kote, na kwenye matokeo ya uhaba wa chakula, joto na maji safi.