1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki Kuu ya Afrika Kusini yamsafisha Ramaphosa

22 Agosti 2023

Benki kuu ya Afrika Kusini imetangaza kuwa Rais Cyril Ramaphosa, hakukiuka kanuni za kubadilisha fedha za kigeni baada ya takriban dola milioni 4 za Marekani kukutwa zimefichwa kwenye sofa lake.

https://p.dw.com/p/4VRAc
Uchunguzi ulihusiana na wizi katika shamba la mifugo la rais huyo tajiri miaka mitatu iliyopita.
Uchunguzi ulihusiana na wizi katika shamba la mifugo la rais huyo tajiri miaka mitatu iliyopita.Picha: Stanislav Krasilnikov/TASS/dpa/picture alliance

Ni kutokana na uchunguzi wa takriban dola milioni 4 za Marekani zilizokutwa zimefichwa kwenye sofa lake.

Benki hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kufanya uchunguzi kwa mwaka mmoja.

Uchunguzi huo ulihusiana na wizi katika shamba la mifugo la rais huyo tajiri miaka mitatu iliyopita.

Ilifahamika kwamba Ramaphosa alikuwa ameficha dola takribani milioni 4 ndani ya sofa.

Wakati wa uchunguzi, Rais huyo alijichanganya mwenyewe kuhusu chanzo cha fedha hizo.

Lakini baadae alikiri kupokea mamilioni ya Dola mwaka 2019 baada ya kuuza Nyati 20 kwa mfanyabiashara wa Sudan.