1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki kubwa Afrika Kusini yakubali kusamehe kwa muda madeni

4 Mei 2020

Wakopeshaji wakubwa nchini Afrika Kusini, Absa wamesema wamekubali kuwasamehe kwa muda ulipaji wa madeni ya mamilioni ya dola wadai wakopaji baada ya sekta hiyo kusema watu milioni 1.2 wametuma maombi ya kutaka msaada

https://p.dw.com/p/3bkh8
Coronavirus Südafrika Township Khayelitsha bei Kapstadt Ausgangssperre
Picha: Reuters/M. Hutchings


Wakopeshaji wakubwa nchini Afrika Kusini, Absa wamesema kwamba wamekubali kuwasamehe kwa muda ulipaji wa madeni ya mamilioni ya dola wadai wakopaji baada ya sekta hiyo kusema watu milioni 1.2 wametuma maombi ya kutaka msaada.

Athari za kufungwa kwa shughuli za kibinadamu nchini Afrika Kusini ,nchi yenye watu milioni 58, wengi masikini,inatarajiwa kuwa kubwa.

Uchumi wa taifa hilo tayari umetumbukia katika mdororo tokea mwishoni mwa mwaka 2019 na kiwango rasmi cha wasiokuwa na ajira kikifikia kiasi asilimia 30.

Absa ambayo ni moja kati ya taasisi nne kubwa za ukopeshaji imesema zaidi ya wateja 376,000 kati ya wateja wake wameomba msaada na benki hiyo itatoa msaada wa randi bilioni 5.8 kutowa afueni ya kurudisha mkopo au kupunguza madeni hayo kwa awamu katika kipindi cha miezi mitatu.