1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bellingham: Natumai nimewafunga mdomo wakosoaji

1 Julai 2024

England wamefuzu robo fainali baada ya kuponea chupuchupu mikononi mwa Slovakia walipopata ushindi wa 2-1.

https://p.dw.com/p/4hkCD
Fußball-EM 2024 | Achtelfinale | England vs. Slowakei | Jude Bellingham erzielt Ausgleichstreffer
Jude Bellingham akifunga goli la kusawazisha dhidi ya SlovakiaPicha: John Sibley/REUTERS

Sehemu kubwa ya mashabiki wa England licha ya kufuzu, hawajaridhishwa na kiwango cha kandanda kilichooneshwa na timu yao ambayo ilikuwa ni mojawapo ya zile zilizokuwa zinapigiwa upatu kuibuka na ubingwa.

Vijana hao wa Gareth Southgate walizomewa na mashabiki wao katika muda wa mapumziko wa mechi hiyo ya Jumapili na katika kipindi cha pili waliokolewa na bao la Jude Bellingham, sekunde 85 tu kabla muda wa ziada wa mchezo huo kukamilika.

Na baada ya kufunga bao hilo, Jude Bellingham ambaye amekosolewa na mashabiki wengi waliotarajia kuona mchezo mzuri zaidi kutoka kwake, amesema anataraji kuwa sasa ametoa jawabu kwa wakosoaji wake.

"Kuichezea England ni jambo zuri sana ila pia ni shinikizo kubwa. Unasikia watu wengi wakizungumza takataka na ni vyema kwamba ukicheza vizuri, unaweza kuwapa jawabu," alisema Bellingham.

Vyanzo: Reuters/DPAE