1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELFAST : IRA yateketeza silaha zake zote

27 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEXK

Tume ya kimataifa inayoyakanisha mchakato wa amani wa Jeshi la Ukombozi la Ireland IRA huko Ireland ya Kaskazini imethibitisha kwamba kundi hilo limeteketeza silaha zake zote.

Generali mstaafu wa Canada John de Chastelain amewaambia waandishi wa habari mjini Belfast kwamba idadi ya silaha zilizoteketezwa zinaoana kabisa na makadirio ya silaha za IRA yaliyotolewa na serikali.Gerry Adams kingozi wa kitengo cha kisiasa cha IRA Sinn Fein amesema hatua hiyo ni ya kijasiri wakati Waziri Mkuu wa Ireland Bertie Ahern ameielezea kuwa ni tukio la kihistoria.Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema anatumai hatua hiyo itapelekea kuchukuliwa zaidi kwa hatua za amani katika kukomesha mkondo wa umwagaji wa damu wa zaidi ya miongo mitatu.

Hata hivyo kiongozi wa chama cha Kirprotestanti katika jimbo hilo la Ireland Ian Paisley ameishutumu repoti hiyo kuwa ina dosari kwa undumila kuwili na kutoaminika kutokana na ukosefu wa ushahidi wa picha.