1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Umoja wa Mataifa wachunguza mauaji ya Hariri

27 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFam

Wapelelezi wa Umoja wa Mataifa wamelitembelea eneo la mripuko wa bomu uliomuuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.

Timu hiyo inayoongozwa na afisa polisi wa Ireland imekaguwa barabara inayopakana na bahari ambapo msafara wa Hariri uliripuliwa hapo tarehe 14 mwezi wa Februari.

Wakati huo huo mjumbe wa Marekani amewasili mjini Beirut kwa ziara ya kushinikiza kuondolewa kwa wanajeshi wote wa Syria walioko nchini Lebanon.