1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Uchunguzi wa kimataifa kuanza juu ya kifo cha Rafik Hariri.

8 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFPO

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limeamuru kuanzishwa kwa uchunguzi wa kimataifa juu ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri aliyeuwawa huko Beirut nchini Syria.

Azimio hilo litakalopata ufadhili kutoka Marekani, Ufaransa na Uingereza limepitishwa bila kupingwa na wawakilishi 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Uchunguzi wa awali tayari unainyooshea kidole cha lawama Syria kwa mauaji hayo.

Syria ambayo imekuwa na majeshi yake nchini Lebanon kwa miongo mitatu sasa imeahidi kuyaondosha majeshi yake kufikia mwisho wa mwezi April.