1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT. Kamati ya umoja wa mataifa yawatia watano mbaroni

31 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEfl

Kamati ya umoja wa mataifa iliyokuwa ikichunguza kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri imewatia kizuizini washukiwa watano hadi kufikia sasa.

Watu hao watano ni miongoni mwa watu walioshikilia vyeo vya juu katika serikal ya Lebanon, iliyokuwa ikiungwa mkono na Syria na watatu kati ya hao ni kutoka idara ya ulinzi.

Hii ni mara ya kwanza kwa kamati hiyo ya umoja wa mataifa kuwahusisha watu waliokuwa na uhususiano wa karibu na serikali ya Syria katika mauaji ya rafik Hariri yalioleta fujo na maandamano ya kila aina na hatimae kusababisha majeshi ya syria kuondoka nchini Lebanon.