1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing.China yaipigia debe Ujerumani kuwa na wajibu mkubwa zaidi katika umoja wa mataifa.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNK

China leo imekubali kuunga mkono nafasi ya Ujerumani kuwa na wajibu mkubwa zaidi katika katika umoja wa mataifa , lakini ikarudia msimamo wake kuwa inapinga dhidi ya kuharakisha upanuzi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Qin Gang amekaririwa na shirika la habari la nchi hiyo akisema kuwa serikali yake inaunga mkono Ujerumani kuwa na wajibu mkubwa zaidi katika umoja wa mataifa na mashirika ya kimataifa. Qin amesema kuwa ujerumani ni mwanachama muhimu katika jumuiya ya Ulaya na kutokana na ufuasi wa nchi hiyo wa maendeleo kwa njia ya amani, Ujerumani inanafasi kubwa katika masuala ya kimataifa, hali ambayo inatambulika na jumuiya ya kimataifa.