1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Mzozo wa kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya bado haujapata ufumbuzi

29 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEgP

Ujumbe wa wawakilishi wa biashara wa Umoja wa Ulaya umeondoka leo mjini Beijing, baada ya siku nne za mazungumzo yaliyolenga kumaliza mzozo wa kibiashara na China. Msemaji wa umoja wa Ulaya hata hivyo amesema mazungumzo hayo huenda yakaendelea.

Kamishna wa biashara wa umoja huo, Peter Mandelson amesema anapanga kuwasilisha pendekezo lake kwa mataifa wanachama wa jumuiya ya Ulaya baadaye leo. Hakuyataja yaliyomo katika pendekehzo hilo lakini anasema ikiwa pendekezo hilo litakubaliwa, litauruhusu umoja wa Ulaya kuanza tena kununua vitambaa na nguo kutoka China katika kipindi cha mwezi mmoja.

Tani kadhaa za nguo kutoka China zimezuiliwa kuingia ndani ya umoja wa Ulaya kwa sababu China tayari imepitisha kiwango kilichowekwa na umoja wa Ulaya mwezi Juni. Kiwango hicho kiliwekwa baada ya viwango vya kimataifa vya uuzaji wa nguo kufutiliwa mbali.