1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING Mugabe kuzuru China

18 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtT

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe atasafiri kwenda nchini China Jumamosi ijayo. Katika ziara hiyo rasmi Mugabe atafanya mazugumzo na viongozi wakuu serikalini akiwemo rais Hu Jintao.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirila la habari la Xinhua, Mugabe ambaye hatua yake ya kuyavunja makazi yasiyo halali imekosolewa vikali, ataitembelea China kwa siku sita.

Kufuatia vikwazo na kutengwa na mataifa ya magharibi, Mugabe sasa ameyageukia mataifa ya Asia, hususan China, Malaysia na Singapore, kujaribu kuanzisha uhusiano mpya na mataifa hayo. Mara ya mwisho Mugabe aliitembelea China mwaka wa 1999.