1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING. China yatakiwa ijieleze juu ya utaratibu wake wa kutoa hukumu ya kifo

2 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEf3

Kamishna wa maswala ya haki za binadamu wa umoja wa mataifa bibi Louise Arbour ameitaka China itoe habari juu ya utaratibu wake wa kutoa adhabu ya kifo.

Katika ziara yake ya siku tano nchini China bibi Louise ame elezea wasi wasi wake, kwamba huenda China inakiuka haki za kibinadamu za watu wanao toka kwenye jamii ya walio wachache na hata wenye akili punguani.

Bibi Loiuse pia alikutana na jaji mkuu wa China na vile vile wanaharakati wa haki za binadamu.

China inapitisha adhabu ya kifo kwa maelfu ya watu kila mwaka.