1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yamwinda kiungo wa timu ya England Eric Dier

5 Januari 2024

Bayern Munich inammezea mate kiungo wa timu ya taifa ya England na klabu ya Tottenham Hotspurs Eric Dier.

https://p.dw.com/p/4auMt
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel Picha: Martin Sylvest/AP Photo/picture alliance

Mtandao wa habari za michezo wa Sky nchini Ujerumani umeripoti kuwa Dier mwenye umri wa miaka 29, yuko kwenye rada ya miamba hao wa Ujerumani.

Tovuti inayohusika na tetesi za uhamisho ya Football Insider, imesema kuwa mabingwa hao wa Bundesliga tayari wamefikia makubaliano binafsi na kiungo huyo Muingereza.

Bayern Munich wako sokoni kutafuta wachezaji wapya kujaza nafasi ya beki wa kati kwani Kim Min Jae atakosekana kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kuiwakilisha timu yake ya taifa ya Korea Kusini katika michuano ya Kombe la mataifa ya Asia.

Vyombo vya habari vya Uingereza pia vimeripoti kuwa, beki wa Chelsea Trevoh Chalobah pia anahusishwa na kujiunga na Bayern kwa mkopo.