1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern waanza msimu kwa mguu mzuri

8 Agosti 2022

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamefunga jumla ya magoli 11 kufikia katika mechi zao mbili walizocheza. Kabla Ijumaa walipoilaza Frankfurt magoli 6 waliifunga Leipzig mabao 5 katika mchuano wa Super Cup.

https://p.dw.com/p/4FGme
Fussball DFL Supercup 2022 | RB Leipzig - FC Bayern München - Sadio Mane
Picha: MIS/IMAGO

Hii ni licha ya kuondoka kwa Robert Lewandowski aliyehamia Barcelona. huyu hapa kocha wa Bayern Julian Nagelsmann.

"Hatutegemei mchezaji mmoja, sisi ni Bayern Munich, tusisahau hilo. Kipindi cha kwanza tumecheza vizuri kabisa, kila mmoja alijituma. Bila shaka tuna wachezaji wenye kasi katika safu ya mashambulizi na kwa kweli si rahisi kucheza dhidi yetu," alisema Nagelsmann.