1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern waangukia pua Bochum

14 Februari 2022

Tofauti ya pointi kati ya vinara wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bayern Munich na timu iliyo katika nafasi ya pili Borussia Dortmund kwa sasa ni pointi sita tu baada ya VfL Bochum kuwahujumu Bayern Munich mwishoni mwa wiki.

https://p.dw.com/p/470Af
Fußball Bundesliga | FC Bayern München - VfL Bochum
Picha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Bochum waliwacharaza Bayern magoli 4-2 katika uwanja wao wa nyumbani wa Vonovia Ruhrstadion.

Bayern walionekana kuzidiwa maarifa na timu hiyo ambayo imepandishwa daraja msimu huu na magoli yote 4 waliyapata katika kipindi cha kwanza kilichokuwa na msisimko mkubwa.

Fußball Bundesliga | FC Bayern München - VfL Bochum
Beki wa Bochum Cristian Gamboa akisherehekea goli na wachezaji wenzakePicha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Bayer Leverkusen wao walishinda mechi yao kwa magoli 4-2 walipokuwa wakicheza na VfB Stuttgart halafu vibonde Greuther Fürth wakawaadhibu Hertha Berlin 2-1.

Hapo Jumapili Borussia Dortmund walikuwa ugenini katika Mji Mkuu Berlin wakicheza na Union Berlin na waliwazidi nguvu wenyeji wao kwa kuwacharaza 3-0 huku Hoffenheim wakiilemea Bielefeld 2-0.

Siku ya Ijumaa RB Leipzig waliizamisha FC Cologne 3-1 katika mechi iliyochezwa uwanjani Red Bull Arena.

Sasa baada ya matokeo hayo Bayern Munich wako kileleni wakiwa na pointi 52 baada ya 22 huku Borussia Dortmund wakiwafuata na pointi 46 nao Leverkusen wako nyuma yao na pointi 41 halafu Leipzig ni wanafunga nafasi za kushiriki Champions League wakiwa na pointi 34.

Ila mbali na Leipzig kuna timu zengine zilizo na pointi 34 nazo ni Hoffenheim, Freiburg na Union Berlin. Augsburg, stuttgart na Greuther Fürth ndizo timu zilizo chini katika jedwali na zilizo kwenye hatari ya kushushwa daraja.