1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kumenyana na Barcelona robo fainali ligi ya Mabingwa

Deo Kaji Makomba
14 Agosti 2020

Itakuwa patashika nguo kuchanika wakati mabingwa wa soka Ujerumani Bayern Munich watapaomenyana na Barcelona ya Uhispania ktika robo fainali nyingine ya champions League Ijumaa.

https://p.dw.com/p/3gzMo
Fußball UEFA Champions League I FC Bayern Muenchen v Chelsea FC I Tor
Picha: Reuters/M. Dalder

Baada ya Klabu ya soka ya RB Leipzig inayoshiriki ligi kuu ya soka ya Ujerumani Bundesliga kutinga hatua ya nusu fainali ya ligi ya Mabingwa wa kandanda barani Ulaya Alhamisi, Mabingwa wa ligi kuu ya soka ya Bundesliga Bayern Munich, wanaonekana kuwa nafasi ya kuungana nao wakati watakapokabiliana uso kwa uso na klabu ya Barcelona ya Uhispania Ijumaa hii. Majogoo hao wawili wa soka barani Ulaya wana historia, Bayern wako katika kiwango kizuri lakini Barcelona wakijivunia kuwa na mshambuliaji machachari Lionel Messi.


Thiago Alcantara wa Bayern hatakuwa kiungo anayecheza dhidi ya timu yake ya zamani jioni hii, na Arturo Vidal akiwa na uwezekano wa kuwemo katika kikosi cha Barcelona dhidi ya Bayern kwa mara ya kwanza tangu aachane na mabingwa hao wa Bundesliga wa mwaka 2018. Mchezaji huyo raia wa Chile anamchukulia Robert Lewandowski kama tishio kubwa. Lewandowski, mshambuliaji raia wa Poland ana uhakika kwa kushinda kiatu cha dhahabu katika ligi ya mabingwa msimu huu.
 

Champions League - FC Barcelona v Napoli | Tor Messi
Lionnel Messi akishangili bao la pili la Brcelona dhidi ya Napoli, Agosti 8, 2020.Picha: Reuters/A. Gea

"Lewandowski kiukweli ni mchezaji wa ajabu,” alisema Vidal katika mkutano na waandishi wa habari. "Yeye ni hatari sana na itakuwa ni ngumu sana kukabiliana naye, lakini tutakuwa tayari."


Beki wa kimataifa wa Ufaransa Benjamin Pavard ndiye majeruhi pekee kwa upande wa Bayern na Kingsley Coman akiwa fiti asilimia 100, kulingana na kocha wa Bayern Hansi Flick. Kutokuwepo kwa Pavard kunamaanisha kwamba Joshua Kimmich atasimama katika nafasi ya beki wa kulia na mchezaji Thiago aliyetokea katika chuo cha soka cha Barcelona ataendelea kusimama katika nafasi ya kiungo licha ya tetesi kwamba hivi karibuni atajiunga na klabu ya Liverpool ya Englang.

Kwa upande wa klabu ya Barcelona, mchezaji wa zamani wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele anarejea katika patashika hiyo baada ya kuwa nje kwa muda wa miezi tisa kutokana na jeraha la msuli lililokuwa likimsumbua. Lakini Bosi wa Barcelona Quique Setien anatarajia kupata "labda dakika chache” kutoka kwa mfaransa huyo.

Chanzo: DW