1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern sasa wamtaka Nagelsmann

26 Aprili 2021

Sherehe za Bayern Munich kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani kwa msimu wa tisa mfululizo zilikatizwa baada ya kufungwa na Mainz licha ya kuwa mshambuliaji wao Robert Lewandowski alirudi kikosini.

https://p.dw.com/p/3sb2y
Fußball Champions League RB Leipzig - Liverpool | Julian Nagelsmann
Picha: Laszlo Szirtesi/Getty Images

Lewandowski alirudi kutoka kwenye jeraha lililomuweka nje kwenye mechi kadhaa na kufunga bao moja.

Mainz waliwazidi nguvu Bayern na kuebuka kidedea mbili moja.

Na sasa kwa kuwa kocha wao Hansi Dieter Flick ameshaweka wazi kwamba huu ndio msimu wake wa mwisho, macho ya mabingwa hao wa Ujerumani wameyaweka kwa mkufunzi wa RB Leipzig Julian Nagelsmann.