1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich yasisitiza Lewandowski hataondoka

16 Juni 2022

Bayern Munich imesisitiza kwa mara ya pili kwamba Robert Lewandowski hawezi kuondoka na kujiunga na timu nyingine kabla ya mkataba wake kumalizika mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4Coxc
Fußball Bundesliga 34. Spieltag | VfL Wolfsburg - FC Bayern | Robert Lewandowski
Picha: Ronny Hartmann/AFP/Getty Images

Nyota huyo wa Poland mwenye umri wa miaka 33 amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda Barcelona, ​​lakini Bayern wamesisitiza kuwa Lewandowski lazima akamilishe mkataba wake ambao unamalizika Juni 2023.

Mkurugenzi wa Bayern Munich anasemaje?

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Hasan Salihamidzic, aliliambia gazeti la kila siku la Ujerumani la Bild kwamba wakati wa mazungumzo ya simu na Lewandowski siku ya Jumanne "alimweleza waziwazi msimamo wao kuhusu hali ya mkataba wake".

Ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha Barcelona wanataka kulipa ada euro milioni 32 (dola milioni 34) kwa mchezaji huyo bora wa kiume mara mbili wa FIFA.

Rais wa Bayern Herbert Hainer

Rais wa Bayern Herbert Hainer alisema hivi karibuni kuwa"Mkataba ni mkataba, tunaenda wapi ikiwa mchezaji anaweza kumaliza mkataba mapema?"

Hata hivyo, mshambuliaji huyo alisisitiza tena mapema wiki hii alipo zungumza akiwa Poland kwa kusema "Ninaondoka kwa sababu ninataka chanagamoto zaidi maishani mwangu

Je! Lewandowski ana hofu?

Bila kuwataja, Lewandowski alidai mabosi wakuu wa klabu yake hawakutaka kunisikiliza hadi mwisho. Alisema "kitu kilichopo ndani yangu kikilitoka nje. Haiwezekani kupuuza".

Baada ya kuitumikia kwa miaka minane Bayern  Munich, Lewandowski ameisaidia clab hiyo kushinda kila taji linalowezekana ikiwa ni pamoja na kubeba taji la Ligi ya Mabingwa mnamo 2020.

Amekuwa mfungaji bora wa Bundesliga kwa kila misimu katika misimu mitatu iliyopita, lakini Lewandowski anaamini kwamba Bayern wanapaswa kumwachilia sasa na kupokea ofa hiyo kutoka  Barcelona badala ya kuondoka mwakani kwa uhamisho wa bure.

Chanzo:AFP