1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayer Leverkusen kukipoiga na Stuttgart DFL-SUPER CUP

16 Agosti 2024

Bayer Leverkusen itaikaribisha Stuttgart katika mechi ya kihistoria ya DFL-Supercup siku ya Jumamosi.Mechi ya kwanza ya ufunguzi wa msimu tangu 1993 bila kuzishirikisha timu za Bayern Munich na Borussia Dortmund.

https://p.dw.com/p/4jYtB
Bundesliga: Bayer 04 Leverkusen - VfB Stuttgart
Bayer Leverkusen wanawakaribisha Stuttgart katika mchezo wa kuwania kombe la DFL-Super CupPicha: nordphoto GmbH / Meuter/picture alliance

 Bayer Leverkusen iliyovunja rekodi msimu uliopita itaikaribisha Stuttgart katika mechi ya kihistoria ya DFL-Supercup siku ya Jumamosi, ikiwa ni mechi ya kwanza ya ufunguzi wa msimu tangu 1993 bila kuzishirikisha timu za Bayern Munich na Borussia Dortmund.

Rekodi hiyo ya miaka 31 inaonyesha jinsi msimu uliopita ulivyokuwa mzuri katika soka la Ujerumani. Kombe hilo la Super Cup la Ujerumani ni sawa na Ngao ya Jamii ya FA ya Uingereza, Mara zote huwakutanisha mabingwa wa Bundesliga dhidi ya washindi wa Kombe la Ujerumani au timu inayoshika nafasi ya pili ya ligi.

Soma zaidi. Leverkusen kuvaana na Stuttgart kuwania Kombe la Supercup

Leverkusen, kwa miongo kadhaa walikuwa wakipewa jina la 'Neverkusen' kama washindi wa pili wa kudumu wa kandanda ya Ujerumani, walishinda taji lao la kwanza kabisa la Bundesliga kwa mtindo wa kuvutia.

Bayer 04 Leverkusen
Kocha wa Leverkusen, Xabi AlonsoPicha: Federico Gambarini/dpa/picture alliance

Kikosi cha Xabi Alonso kiliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza katika historia ya Ujerumani kushinda ligi hilo bila kufungwa, rekodi ambayo imewakwepa hata mabingwa mara 33 Bayern Munich.

Leverkusen pia ilishinda Kombe la Ujerumani na kufika fainali ya Ligi ya Europa na kupoteza kwao 3-0 dhidi ya Atalanta kwenye fainali ambayo iliwafanya kupoteza mchezo pekee katika michezo 53 waliyocheza msimu uliopita.

Xhaka: Tumejiandaa vya kutosha

Granit Xhaka, kiungo muhimu na injini kwa eneo la kiungo la Leverkusen, ameliambia shirika la habari la AFP katika mahojiano kwamba  mafanikio waliyoyapata msimu uliopita bado hayaridhidhi na kwamba wataendelea kupambana kwa mataji zaidi.

 "Tuko nyumbani dhidi ya timu nzuri sana, kwa hakika, lakini kwa mashabiki wetu, wafuasi wetu, ninaamini tunaweza kushinda kombe kwa msimu wetu, kuchukua hatua ya kwanza," alisema mchezaji Xhaka.

 Granit Xhaka
Nahodha na kiungo wa Bayer Leverkusen Granit Xhaka amesema wamejiandaa vya kutosha kuelekea mchezo huo na wanahitaji kulibeba kombe la DFL-Super CupPicha: Anke Waelischmiller/Sven Simon/picture alliance

Soma zaidi. Alonso ahisi fahari na uchungu baada ya 'Neverlusen' kushindwa
Mshambulizi mpya wa Stuttgut Ermedin Demirovic, ambaye amechukua nafasi ya Serhou Guirassy aliyetimkia Dortmund, alisema siku ya Alhamisi kuwa mechi yao na Leverkusen itatoa picha ya kikosi chao kuelekea msimu mpya. "tutafanya kila kitu kushinda mchezo huo"amesema Demirovic.

 Bayer Leverkusen haijawahi kushinda Supercup, Mwaka 1993 walipoteza kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Werder Bremen katika mechi yao ya fainali pekee.Kwa upande wa Stuttgart wao wamewahi kulitwaa taji hili la Supercup mara moja, walipoifunga Hannover 3-1 mnamo 1992.

Mechi ya Bayer Leverkusen na Stuttgart itachezwa majira ya saa tatu na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki katikia dimba la Bay Arena.