1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baver Leverkusen yapipanga kuikwaa Bayern Munich

9 Februari 2024

Kocha ya klabu ya mpira ya Bayer Lerverkusen, Xabi Alonso, amesema timu yake inahitaji kuwa imara kuweza kuishinda Bayern Munich kesho Jumamosi, licha ya wasiwasi wa mabingwa hao wa Ujerumani kuhusu majeruhi.

https://p.dw.com/p/4cEX7
Xabi Alonso na Thomas Tuchel
Xabi Alonso na Thomas TuchelPicha: Frank Hoermann/SVEN SIMON/Revierfoto/dpa/picture alliance

Alonso, ambaye alishinda kombe la dunia na Champion's League pamoja na mataji ya ligi kadhaa wakati akizichezea klabu za LIverpool, Real Madrid, Bayern Munich na Uhispania, ameahidi kutumia uzoefu wake huo wa mechi kubwa kuwafunga mahasimu wao.

Lakini ameelezea hofu ya wachezaji wake kwa mshambuliaji wa Bayern, Harry Kane, ambaye amefunga mabao 24 katika mechi 20 za Bundesliga, tangu kujiunga na Bayern akitokea Tottenham ya Uingereza.