1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barrack Obama na mkewe wamuidhinisha Harris kugombea urais

26 Julai 2024

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama, wamemuidhinisha makamu Rais wa nchi hiyo Kamala Harris kugombea urais wa nchi hiyo wakati wa uchaguzi wa mwezi Novemba.

https://p.dw.com/p/4inBG
USA Washington 2022 | Kamala Harris und Barack Obama lauschen Joe Bidens Rede zur Gesundheitsreform
Picha: Chris Kleponis/CNP/ABACA/picture alliance

Hatua hiyo inampa Harris uungwaji mkono muhimu wa wanachama hao wawili maarufu wa chama cha democratic nchini humo.

Rais huyo wa zamani amemwambia Harris kwamba yeye na mkewe wana furaha kumuidhinisha na kuahidi kufanya wawezalo kuhakikisha anapata ushindi.

Kamala Harris aashiria mabadiliko makubwa kwenye sera ya Marekani kuhusu Gaza.

Uidhinishaji huo, uliotangazwa leo asubuhi, unakuja wakati ambapo Harris anaendelea kupata uungwaji mkono kama mteule wa chama hicho cha Democratic kugombea urais baada ya uamuzi wa Rais Joe Biden kusitisha azma yake ya kugombea tena na kumuidhinisha makamu huyo wake.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la Associated Press, Harris tayari amepata uungwaji mkono wa umma wa wajumbe wengi wa kongamano la kitaifa la chama hicho cha Democratic litakaloanza Agosti 19, jimboni Chicago.