1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barcelona hoi dhidi ya Madrid

17 Oktoba 2022

Barcelona wamepata machungu mara mbili kwa kuwa hapo Jumapili walifungwa kwa mara ya kwanza msimu huu katika Ligi Kuu ya Uhispania La Liga.

https://p.dw.com/p/4IIEF
UEFA Champions League Real Madrid vs Shakhtar Donetsk
Picha: Denis Doyle/Getty Images

Na kipigo hicho cha 3-1 wamekipata mikononi mwa watani wao Real Madrid katika mechi yenye umuhimu mkubwa ya El Clasico.

Karim Benzema, Federico Valverde na Rodrygo ndio waliowafungia Madrid mabao yao matatu. Kushindwa huko ni pigo kwa kocha wa Barca Xavi ambaye timu yake pia iko karibu kubanduliwa kutoka kwenye ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya.

Xavi alikuwa na haya ya kusema baada ya mpambano huo.

Fußball Katar | Trainer Al Sadd SC Xavi Hernandez
Xavi HernandezPicha: Nikku/XinHua/picture alliance

"Nina wasiwasi kwa kuwa hatuko katika kiwango chetu. Tumepambana na timu nzuri inayojua kucheza isiyojali iwapo itajilinda au kushambulia, hatukufaa kukubali kufungwa goli la kwanza jinsi lilivyofungwa, tulihitaji hata kuwachezea rafu kwasabau tulikwenda mapumzikoni tukiwa tumefungwa magoli 2. Kwa hiyo Real Madrid walitumia nafasi ya mashambulizi ya counter tuliyowapa na wakati mwengine katika kandanda hata kama huchezi vizuri ila ukitumia nafasi zako vyema unaweza kupata hata sare," alisema Xavi.

Naye kocha wa Madrid carlo Ancelotti amefurahia ushindi huo ila anasema hakuna cha ziada ni pointi tatu tu walizozishinda.

UEFA Champions League Finale | Liverpool FC vs Real Madrid
Carlo AncelottiPicha: Adam Davy/PA Wire/dpa/picture alliance

"Nafikiri kipindi cha kwanza ndicho kilichotufanya tushinde mechi kwasababu tulikuwa bora na tulizitumia nafasi zetu. Nafikiri tuliwadhibiti vyema kutoka kwenye safu yetu ya ulinzi kwasababu walilenga kutuwekea shinikizo ila tukawa tunaelekea upande wao na kujiamini. Tulijilinda vyema kwasababu tulishirikiana kama timu. Kwa hiyo nafikiri kipindi cha kwanza ndicho kilichoamua mechi," alisema Ancelotti.

Kwa ushindi huo Madrid wanaiongoza La Liga sasa wakiwa na pointi 25 tatu mbele ya Barca kisha Atletico Madrid ambao walipata ushindi wa bao moja lililofungwa na Antoine Griezmann walipokuwa wakicheza na Athletic Bilbao, kwa sasa wako katika nafasi ya tatu na pointi 19.