1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Seneti Marekani lapitisha msaada kwa Ukraine

13 Februari 2024

Baraza la Seneti la Bunge la Marekani Jumanne limepitisha muswada wa dola bilioni 95.3 unaojumuisha msaada zaidi kwa Ukraine, Israel na Taiwan, licha ya hofu ya kupingwa mbele ya Baraza la Wawakilishi la nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4cM3x
USA US-Repräsentantenhaus Wahlen
Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Baraza hilo linalodhibitiwa na chama cha Democratic cha Rais Joe Biden limeuridhia muswada huo kwa kura 70 dhidi ya 29 zilizoupuinga na kuupeleka rasmi mbele ya Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na chama cha Republican.

Hata hivyo, tayari kuna mashaka kuwa muswada huo hautapata kura za kutosha kwenye Baraza hilo, baada ya Warepublican kusema haujajumuisha hatua za kuzuia wimbi la wakimbizi wanaoingia Marekani ambazo walizipendekeza kama sharti la kuuunga mkono.

Ukraine ndiyo hasa inasubiri kwa shauku hatma ya muswada utakaowezesha kupatiwa msaada zaidi wa silaha na fedha kuendelea na vita dhidi ya Urusi.