1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maseneta wazuia muswaada wa matumizi kwa Ukraine na Israel

7 Desemba 2023

Baraza la Seneti la nchini Marekani limeuzuia muswada wa matumizi ya dharura mabilioni ya dola ambayo ingetumika kuisaidia kiusalama Ukraine na Israel.

https://p.dw.com/p/4ZrkH
Abstimmung der Abgeordneten über McCarthy
Picha: Win McNamee/AFP/Getty Images

Hatua hiyo inafanyika huku wabunge wa Republican wakishinikiza hatua kali zaidi za kudhibiti uhamiaji katika mpaka kati ya Marekani na Mexico.Wabunge 49 waliunga mkono na 51 waliupinga muswada huo, hii iikiwa ni upungufu wa kura 60 zilizotakiwa ili kusonga mbele, hali inayoibuamashaka kuelekea mpango wa Rais Joe Biden wa kutoa msaada mpya kabla ya mwishoni mwa mwaka huu.Iwapo ungepitishwa, Marekani ilinuia kutoa dola karibu bilioni 50 kama msaada mpya wa ulinzi pamoja na fedha za misaada ya kiutu kwa serikali ya Kyiv, na dola bilioni 14 kwa Israel inayopambana na Hamas.