1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Baraza la mpito la Haiti lateua baraza jipya la mawaziri

12 Juni 2024

Baraza la mpito la Haiti limeteua baraza jipya la mawaziri, ikiwa ni hatua ya mwisho ya kujenga upya serikali itakayoongoza taifa hilo lililozingirwa na magenge ya uovu.

https://p.dw.com/p/4gw9F
Haiti Port-Au-Prince | Garry Conille
Garry Conille anahudhuria sherehe na wajumbe wa baraza la mpito ambapo anakuwa kama Waziri Mkuu wa muda wa Haiti, huko Port-au-Prince, Haiti Juni 3, 2024Picha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Miongoni mwa walikuwemo katika baraza hilo ni Carlos Hercules, ambae alikuwa mwanasheria katika ofisi ya Waziri Mkuu Garry Conille,ameteuliwa kuwa waziri wa sheria na usalama wa umma. Jean Marc Berthier Antoine, waziri wa ulinzi.Haiti inakabiliana na magenge ambayo yanadhibiti takriban asilimia 80 ya mji mkuu ya Port au Prince. Majuma kadhaa ya machafuko yalisababisha mwezi Aprili Waziri Mkuu wa Zamani Ariel Henry kujiuzulu. Zaidi ya watu 2,500 waliuawa au kujeruhiwa katika kipindi cha kwanza cha miezi mitatu ya mwaka, na zaidi ya nusu milioni kuachwa bila ya makazi.