1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Mawaziri la Nigeria kuamua hatima ya Rais YarÁdua

23 Januari 2010

Mwanasheria Mkuu wa Nigeria Michael Aondoakaa amesema baraza la mawaziri litaamua iwapo afya ya Rais Umaru YarÁdua inamruhusu kuiongoza nchi baada ya kuwa nje kwa matibabu tangu miezi miwili iliyopita.

https://p.dw.com/p/Lewr
Umaru Musa Yar'Adua (* 1951 in Katsina) ist ein nigerianischer Politiker und seit 2007 Staatspräsident Nigerias. Umaru Yar'Adua, waits to make his acceptance speech after he was declared winner at the People's Democratic Party (PDP) primary elections in Abuja, Nigeria, Sunday, Dec. 17, 2006. Nigeria's ruling party on Sunday chose a Muslim from the north as its candidate in next year's presidential elections. Governor Umaru Yar'Adua of Katsina, had won 3,024 votes _ easily beating his closest rival, who received only 372 votes. (AP Photo/George Osodi)
Rais Umaru Musa YarÁdua wa Nigeria.Picha: AP

Kiongozi huyo mwenye miaka 58 hakuonekana hadharani tangu mwezi wa Novemba alipokwenda Saudi Arabia kwa matibabu ya moyo. Jaji Dan Abutu amelitaka baraza la mawaziri kupitisha uamuzi wake kuhusu afya ya rais YarÁdua katika kipindi cha siku kumi na nne. Hatua hiyo inachukuliwa baada ya mbunge mmoja wa zamani kuishtaki serikali kuwa imekwenda kinyume na katiba ya nchi kwa kutomkabidhi madaraka kiongozi mwengine.

Mapema mwezi wa Desemba,baraza la mawaziri kwa kauli moja lilikubaliana kuwa hakuna sababu ya kumtaka Rais YarÁdua kujiuzulu. Mawaziri hao walipinga mito ya kumtaka ajiuzulu au kuthibitisha iwapo afya yake inamruhusu kubakia madarakani.

Baadhi ya wachambuzi wanasema,mawaziri wanasita kumpinga YarÁdua kwa sababu ya kuhofia kuwa watapoteza kazi zao ikiwa Makamu wa Rais Goodluck Jonathan atakabidhiwa madaraka.

Mwandishi:Martin,Prema/RTRE

Mhariri: Kitojo,Sekione