1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaidhinisha makubaliano ya kuachiliwa huru mateka

22 Novemba 2023

Baraza la mawaziri la Israel limepiga kura ya kuidhinisha makubaliano ambayo yatatoa nafasi ya kuachiliwa kwa baadhi ya mateka waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo la Hamas mnamo Oktoba 7.

https://p.dw.com/p/4ZHul
Israel Tel Aviv  Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Xinhua/IMAGO

Mkutano huo wa baraza la mawaziri umefanyika baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuitisha mkutano na baraza lake la mawaziri maalum kwa ajili ya vita na usalama.

Kuelekea kura hiyo ya kuidhinisha makubaliano ambayo yatatoa nafasi ya kuachiliwa kwa baadhi ya mateka, Netanyahu amesema serikali ilikuwa inakabiliwa na uamuzi mgumu, lakini anaunga mkono makubaliano hayo.

Netanyahu ameashiria uwezekano wa "kuwa na habari njema hivi karibuni" juu ya makubaliano ya kuwaachila huru mateka, makubaliano ambayo Marekani imesema yako karibu kuafikiwa.

Maelezo kamili ya makubaliano hayo bado hayajatolewa rasmi ingawa ripoti za vyombo vya habari zinaeleza kuwa mateka kadhaa huenda wakaachiliwa huru kama sehemu ya kusitisha vita katika ukanda wa Gaza.