1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Katiba Senegal lafuta uamuzi kuahirisha uchaguzi

16 Februari 2024

Baraza la Katiba la Senegal limebatilisha tangazo la kuchelewesha uchaguzi wa rais uliokuwa ufanyike mwezi huu.

https://p.dw.com/p/4cT6r
Moto ukiwaka kufuatia maandamano ya upinzani nchini Senegal.
Moto ukiwaka kufuatia maandamano ya upinzani nchini Senegal.Picha: Seyllou/AFP

Uamuzi huo wa kihistoria unazidisha suintafahamu katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo kijadi limekuwa na utulivu. 

Baraza hilo la Katiba limesema muswada uliopitishwa na bunge wa kuchelewesha uchaguzi ulikuwa kinyume na katiba, kulingana na nyaraka iliyothibitishwa na chanzo kimoja ndani ya taasisi hiyo. 

Baraza hilo pia liliwahi kubatilisha agizo la Rais Macky Sallla Februari 3 ambalo lilikuwa limebadilisha ratiba ya uchaguzi wiki tatu tu kabla ya kupiga kura.

Soma zaidi: Wabunge wakamatwa wakipinga kuahirishwa uchaguzi Senegal

Uamuzi wa kuchelewesha uchaguzi, ambao awali ulikuwa ufanyike Februari 25, umeitumbukiza Senegal katika mzozo mbaya wa kisiasa na kuchochea hasira ya umma na maandamano ya vurugu.

Upinzani na makundi ya asasi za kiraia yalikuwa yameitisha maandamano mapya siku ya Ijumaa (Februari 16) .