1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Afrika ya Kati

Bangui wapiga kura kubadilisha katiba

30 Julai 2023

Raia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameanza kupiga kura ya maoni ya katiba mpya itakayomfungulia njia rais Faustin-Archange Touadera kugombea awamu ya tatu.

https://p.dw.com/p/4UYTs
Zentralafrikanische Republik | Referendung
Picha: Barbara Debout/AFP/Getty Images

Karibu raia milioni 1.9 wanashiriki kura ya mapendekezo ya mabadiliko hayo yatakayoongeza mamlaka ya rais kutoka miaka mitano hadi saba na kuondoa ukomo wa awamu mbili.    

Mwaka 2020, Touadera alishinda awamu ya pili hadi mwaka 2025, baada ya uchaguzi kuvurugwa na baadhi ya makundi ya waasi wenye silaha, lakini pia uliokabiliwa na madai ya udanganyifu.

Wapinzani wake sasa wanamshutumu kwamba anataka kuwa rais wa maisha, chini ya ulinzi unaozidi kuimarika kwa kundi binafsi la wanamgambo la Wagner la nchini Urusi, ambalo kwa mara ya kwanza liliwasili nchini humo mwaka 2018.