1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANDUNG : Afrika na Asia kukuza biashara na kupambana na umaskini

24 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJp

Viongozi wa Asia na Afrika leo wametia saini katika mji wa kishitoria nchini Indonesia ambao miongo sita iliopita ulishuhudia kuudwa kwa Umoja Usiofungama na Upande wo wote Ushirikiano mpya wa Mkakati wa kuhakikisha amani,utulivu na usalama katika mabara hayo mawili kwa kukuza biashara na kuimarisha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi na makundi ya uhalifu ya kimataifa.

Azimio la kurasa nne linaloitwa Ushirikiano Mpya wa Asia na Afrika NAAP limetiwa saini na Rais wa Indonesia Susilo Bambang Yudhoyono na Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini.

Viongozi kutoka nchi 100 za Asia na Afrika wameidhinisha azimio hilo kwenye mkutano wa viongozi wa siku mbili uliomalizika hapo jana mjini Jakarta.

Mkutano wa viongozi wa mwaka 1955 ulikuwa ni mkutano wa kwanza mkubwa wa kile kilichokuja kujulikana kama dunia ya tatu na wanahistoria wanasema ndio uliopelekea kuja kuundwa rasmi kwa Umoja usiofungana na upande wowote hapo mwaka 1961.