1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bale kukamilisha kazi ya soka Madrid

Deo Kaji Makomba
5 Juni 2020

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid ya nchini Uhispania, Gareth Bale, kwa hivi sasa hataki kurejea tena katika ligi kuu ya kandanda ya England, Premier.

https://p.dw.com/p/3dIhQ
Fußball Klub-WM Halbfinale Kshima Antlers - Real Madrid Gareth Bale
Picha: picture-alliance/Zumapress/M. Dominguez

Kauli hiyo ya Bale kubaki katika klabu ya Real Madrid imetolewa na wakala wake, Jonathan Barnett.

Licha ya kushinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya akiwa na Real, Bale amegawa maoni ya mashabiki na wachambuzi wa soka kufuatia ushiriki wake hafifu na kuwa na rekodi mbaya ya majeraha. Alionekana kuwa tayari kwa harakati ya kuhamia katika klabu ya China Jiangsu Suning mwaka jana kabla ya mpango huo kushindwa kutimia.

"Ana maisha mazuri. Sioni kwa nini aangazie kazi yake nje ya Madrid, Barnett aliimbia BBC. "Kurudi tena kucheza kwenye Ligi Kuu itakuwa ni jambo kubwa la kushangaza. Sidhani kama anataka kufanya hivyo kwa sasa. Ana furaha sana kucheza huko Real."

Na Deo Kaji Makomba/Reuters