1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAKU :Maafisa wafukuzwa kazi Azerbaijan kutokana na udanganyifu

10 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJy

Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan amewafukuza kazi maafisa wawili kutokana na kuhusika na udanganyifu katika uchaguzi wa bunge uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.Hatua hiyo inafuatia maandamano makubwa katika mji wa BAKU yaliyofanywa na watu wapatao alfu 15 wanaotaka uchaguzi wa bunge ufanyike upya.Maafisa hao wawili ni magavana wa majimbo.

Waendesha mashtaka wamesema maafisa wengine wanne pia wametiwa ndani kutokana na tuhuma za kujaribu kubadili matokeo ya kura.