1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAHRAIN: Rice aikosoa Syria kuhusu wapinzani

12 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJB

Kwenye mkutano wa “Demokrasia ya Mashariki ya Kati”waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani,Bibi Condoleezza Rice aliitumia fursa hiyo kukosoa ukandamizaji wa kisiasa nchini Syria.Alitoa mwito pia wa kumuachilia huru mwana harakati wa kisiasa Kamal Labwani,aliekamatwa siku ya Jumanne,kwenye uwanja wa ndege wa Damascus aliporejea kutoka Marekani.Wagombea haki za binadamu wanakisia kuwa nchini Syria kuna wafungwa wa kisiasa wapatao kama 2,500.Akizungumza huko Bahrain,Rice alijaribu kutuliza shaka za Waarabu kuhusika na ajenda ya Marekani juu ya mageuzi katika Mashariki ya Kati.Mkutano wa Bahrain unahudhuriwa na mawaziri na wajumbe wa mashirika yasio ya kiserikali kutoka Mashariki ya Kati,Afrika ya Kaskazini na Ulaya.