1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:mwenyekiti wa kamati ya Olimpiki nchini Irak ametekwa nyara pamoja na watu wengine zaidi ya 50

15 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG7K

Mwenyekiti wa kamati ya Olimpiki ya Irak pamoja na watu wengine kadhaa wametekwa nyara mjini Baghdad.

Polisi ya mji huo imesema kuwa watu waliokuwa na silaha walikivamia kituo cha utamaduni ambapo watu, walikuwa wanashiriki katika mkutano.

Wateka nyara hao waliokuwa wamevaa sare za polisi waliwateka watu zaidi ya hamsini.

Habari zaidi kutoka Baghdad zinesema ,katika sehemu mbalimbali za kusini mwa mji huo majeshi ya usalama yaligundua maiti za watu wapatao 16 waliokuwa wamepigwa risasi.Watu hao walifunikwa nyuso kwa vitambaa na walikuwa wamefungwa pingu.